Jana jumapili tarehe 20/04/2014 kwenye kipindi
cha AMKA NA BADILIKA kupitia TBC1 mada
iliyokuwa ikizungumzwa ilikuwa ikihusu mitandao
ya kijamii. Wageni walikuwa mwakilishi kutoka
TCRA(mamlaka ya mawasiliano) na Bwana Mike
Mushi, mmoja wa waanzilishi wa mtandao
mkubwa Tanzania unaoitwa Jamii Forums.
Walikuwa wakizungumzia changamoto na jinsi
ya kunufaika kiuchumi na mitandao ya kijamii.
Yalizungumzwa mambo mengi sana, lakini moja
lililonigusa sana ni kuhusu kutengeneza fedha
kupitia blogs. Mike Mushi alisema ni vigumu
sana kutengeneza fedha kupitia blog kwa
kutegemea matangazo. Inakubidi uwe na
watembeleaji wengi sana ndio uweze kushawishi
kampuni kubwa iweke tangazo kwenye blog
yako. Na hii ndio imekuwa ikisababisha blog
kuweka habari zisizo na maadili ili kupata
watembeleaji wengi na waweze kupata
matangazo. Mwisho wa siku hawapati hayo
matangazo na heshima yao inashuka sana.
Kitu kingine kinachofanya kutengeneza fedha
kwenye mtandao kupitia blog kuwe kugumu ni
ukosefu wa ubunifu. Kila mtu anayefungua blog
siku hizi anaripoti habari. Kwa njia hii kumekuwa
na kelele nyingi sana kwenye mtandao kitu
ambacho kinawafanya wanaojihusisha na aina
hii ya kublog kuumia sana kichwa kutokana na
kutopata kile walichodhamiria kupata.
Pamoja na yote hayo bado kuna nafasi kubwa
sana ya kuingiza kipato kisicho na kikomo
kupitia blog. Sekta ya utumizi wa mtandao wa
internet hapa kwenye Tanzania bado ni ndogo ila
inakuwa kwa kasi sana. Bado kuna soko kubwa
sana ambalo kama ukiweza kulitumia vizuri
unaweza kuanzisha na kukuza biashara yako
kupitia mtandao. Huduma za malipo kwa
kutumia simu kama mpesa na tigo pesa
zimefanya biashara hii kuwa rahisi zaidi.
Ili kukuondolea adha hii ya kupoteza muda
kwenye mtandao kwa kufanya vitu ambavyo
haviwezi kukulipa, nimekuandalia kozi fupi ya
JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE
MTANDAO KUPITIA BLOG. Kozi hii itakuwa na
vipengele vifuatavyo.
1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za
blog.
2. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia
blog.
3. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua
mtindo wako.
4. Uandishi wa makala zenye mvuto.
5. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi
zaidi(email list).
6. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya
kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.
7. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.
8. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au
huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa
masoko.
9. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia
blog yako.
10. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na
jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.
Kozi hii itafundishwa kwa njia ya mtandao na
itachukua muda wa siku kumi tu. Gharama ya
kozi hii ni shilingi elfu kumi za kitanzania.
Kujiunga na kozi hii tuma fedha(tsh 10,000/=)
na email yako kwa mpesa au tigo pesa
0755953887/0717396253 kisha utaingia kwenye
kozi hii. Kozi itaanza rasmi tarehe 28/04/2014.
Mwisho wa kujiunga na kozi hii ni ijumaa ya wiki
hii tarehe 25/04/2014.
Wahi kujiunga na kozi hii kabla muda
haujaisha. Hatutapokea watu katikati ya kozi.
Hii ni nafasi kubwa sana kwako kuweza
kutengeneza kipato cha uhakika na kisicho na
kikomo. Dunia inabadilika kwa kasi sana na
mtandao wa internet umetengeneza matajiri
wengi sana duniani. Usiachwe nyuma na njia hii
ya kipekee na ya uhuru ya kujiingizia kipato.
Karibu kwenye ukombozi wa maisha yako
kiuchumi.

Categories:

Leave a Reply