Na Charles Nazi
Hali ya uchumi duniani imekuwa ngumu si hapa kwetu Tanzania tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea. Uwezo wa serikali nyingi duniani hasa wa kutoa huduma kwa watu wake unazidi kupungua kutokana na serikali nyingi kuelemewa na madeni. Matatizo yaliyosababisha hali hii ni pamoja na; kushuka kwa thamani ya pesa, kupanda kwa deni la taifa, ongezeko la watu, kupanda kwa bei ya mafuta,makampuni kufilisika na wafanyakazi kupunguzwa kazini na kukosekana kwa elimu ya ujasiriamali kwa jamii. Hali hii inazidi kuwagusa watu wengi zaidi duniani pengo la masikini na matajiri linazidi kuwa kubwa na tabaka la kati linaanza kutoweka. Hali hii ikiendelea kama ilivyo kutakuwa na matabaka mawili tu duniani yaani matajiri na masikini.  Jee unawezaje kuepuka kuingia katika tabaka la umasikini na kuingia katika tabaka la matajiri? Suluhisho ni kuwa mjasiriamali kwa kujifunza na kutekeleza kwa vitendo mbinu za ujasiriamali.
Watu wengine wamekuwa na dhana potofu kwamba tatizo la umasikini linatokana na ukosefu wa pesa au mitaji peke yake lakini mimi nina mtizamo tofauti, kama tatizo la umasikini lingekuwa ni ukosefu wa fedha kuna matajiri wawili kule Marekani, Donald Trump na Robert Kiyosaki wamesema kwamba wangejitolea kuwagawia watu pesa lakini katika utafiti wao wamegundua kwamba hata ukimpa mtu pesa atatumia zikiisha atarudi tena kuja kuomba, hivyo mbinu hiyo siyo endelevu inamfanya huyu anayeomba kuwa tegemezi na kuzidi kuwa masikini. Kwa hiyo walichukua msemo wa kichina kwamba ukitaka kumsaidia mtu uasimpe samaki ila umpe nyavu na mbinu za kuvua samaki. Vivyo hivyo katika kumkomboa mtu kutoka kwenye umasikini unatakiwa kupatia elimu ya ujasiriamali na namna ya kutumia mbinu hizo.  Kwa hiyo watu hawa pamoja na wanaharakati wengine wa kupambana na umasikini tumeamua kutoa elimu ya ujasiriamali kwa kutumia njia mbali mbali. Kwa maoni yetu pesa haikufanyi wewe kuwa tajiri bali elimu ya ujasiriamali ndiyo inayoweza kukufanya kuwa tajiri. Kama pesa ingekuwa inao uwezo wa kuwafanya watu wawe matajiri kuna miofano mingi tu ya watu ambao walipata bahatinasibu ya mamilioni na wastaafu ambao walipata mafao ya mamilioni ya fedha lakini kwa kukosa elimu ya ujasiriamali wametumia pesa zote na kufilisika.
Kila mtu ana matatizo yake ya kifedha  katika dunia ya sasa kuwa na elimu na kuwa na Shahada ya fani fulani pekee haitoshi unatakiwa kuwa na elimu pia ya ujasiriamali, kutegemea pensheni peke yake ni tatizo, kwani utafiti uliofanyika ni kwamba Wastaafu wengi ambao wanategemea pensheni zao huishiwa ndani ya miaka 5 baada ya kustaafu na kulipwa mafao yao ya mkupuo na zile hela za pesheni wanazolipwa  kidogo kidogo kila mwezi  huwa hazitoshi hata kukidhi mahitaji ya muhimu ya watu hao na kuwafanya waishi katika hali ya umasikini. Sizungumzii hali hii kwa nia ya kuwatisha watu  ila hii ndiyo hali halisi kama ukitaka kuthibitisha maneno haya waulize wazee wastaafu watakwambia kuhusu taabu wanazozipata.
 Watu wengine wamekuwa na mawazo ya kuitegemea serikali iwakwamue katika matatizo yao ya kifedha hayo pia ni mawazo potofu. Serikali haiwezi kukutatulia matatizo yako ya kifedha ila ni wewe mwenyewe ndiyo unaweza kutatua matatizo yako ya kifedha kwa kuchukua hatua kupata maarifa ya ujasiriamali, kubuni shughuli za uzalishaji mali utoaji huduma na biashara.  Bahati mbaya hata wajasiriamali tulionao wamekuwa wakiendesha biashara zao kwa mazoea hivyo kuzifanya zisiwe endelevu. Kama wewe ni mjasiriamali wekeza kwenye maarifa ya ujasiriamali pia ili uinue hali yako ya maisha. Unaweza kujiendeleza kwa kusoma vitabu vya ujasiriamali, kusoma makala kama hizi kwenye magazeti, kuhudhuria mafunzo na semina za ujasiriamali ambazo huwa zinatolewa na watu mbali mbali.
Mtaji mkubwa uliopewa na mwenyezi Mungu ni akili yako. Watu wengi hatutumii vizuri akili zetu katka kufikiria namna ya kutatua matatizo yetu, kwa mfano unapopata tatizo lolote badala ya kufikiria kuhusu tatizo hilo anza kufikiria namna ya kutatua tatizo hilo. Pia kama ukimudu kufikiria namna ya  kutatua matatizo yako basi unaweza kuanza kufikiria namna ya kutatua matatizo katika jamii ukisha jua matatizo yanayoikabili jamii unaweza kutafuta suluhisho na hilo suluhisho unaweza kulifanya likawa fursa ya biashara. Kwa mfano kuna mtu mmoja alikuwa anaishi katika kijiji kimoja katika kutafuta mahitaji yake ya kila siku kama vile sukari, majani ya chai unga wangano nk. alilazimika kutembea umbali wa kilomita 3 kila mara ili kwenda kununua mahitaji yake kijiji cha jirani. Alivyochunguza akagundua kwamba tatizo hili lilikuwa si la kwake peke yake hata wanakijiji wenzake walikuwa wakihangaika kufuata bidhaa hizo kijiji cha jirani kama yeye, ndipo hapo jamaa aliamua kuanzisha duka la rejareja katika kijiji chake, na kwa kweli duka lake liliendelea sana na alipata pesa nyingi.   Ili ufanikiwe kiuchumi maishani unapaswa kuwa mtundu, mbunifu na mtafiti.
Eneo lingine ambalo hatulitumii ni kukagua vipaji vyetu. Mwenyezi Mungu kamjalia kila mtu kipaji chake, wengine ni waimbaji wazuri, wasusi, wasanii, wachekeshaji, washereheshaji, wakimbiaji, wapishi wazuri nk. Jee umewahi kijuliza una kipaji gani? Kama hujui waulize watu wako wa karibu, kama vile baba, mama, kaka, dada, rafiki, mke mume nk. Jee unakitumia kipaji chako ipasavyo kukuletea maendeleo yako kiuchumi? Kwa mfano kama wewe ni msusi mzuri kwa nini usianzishe saluni? Kama wewe una kipaji cha kupika kwa nini usianzishe hoteli? Bahati nzuri sana kipaji chako kinaweza kuwa ndiyo mtaji wako mkuu wa kuendesha biashara yako. Muhimu ukigundua kipaji chako lazima ukiendeleze.
Jee unapaswa kufanya nini ili upambane na tatizo hili la umasikini? Kwanza unapaswa kuwa na shuguli ya kufanya. Inasikitisha kuona watu wazima wanakaa vijiweni, kina babu wanashinda kwenye kahawa na kucheza bao siku nzima au vijana wanacheza pool siku  nzima. Mtu yeyote aliyefikisha umri wa miaka 18 anapaswa kuwa na shughuli ya kufanya kama ni ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Jee wewe ni kati ya  watu wengi ambao  wana mitaji lakini hawajui wafanye nini unaweza kutumia akili yako kubuni shughuli ya kufanya au kutumia kipaji chako kufanya biashara. Hatua ya pili ni kujenga tabia ya kuweka akiba. Katika dunia ya sasa kuna sehemu nyingi ambazo unaweza kuweka akiba yako mfano kwernye SACCOS, akaunti za akiba kwenye benki mbali mbali. Unapaswa kuweka kati ya asilimia 10 % hadi 15 % ya mapato yako kwa mwezi. Mwisho ni kuwekeza fedha zako katika vitegauchumi endelevu. Jee ni vitegauchumi gani ambavyo ni endelevu, kuwekeza katika majengo ya kupangisha. Kwa nini tunashauri uwekeze pesa zako katika vitegauchumi ni kwa sababu pesa ikikaa sana benki huwa inaongezeka kidogo kidogo kwani faida inayopatikana ni ndogo kuliko mfumuko wa bei hivyo baada ya muda pesa yako itashuka thamani, lakini ukiwekeza kwenye kitegauchumi endelevu thamani ya pesa yako inapanda. Kwa mfano ukiwekeza kwenye majengo ya kupangisha kila hali ya uchumi inavyozidi kuwa mbaya thamani ya majengo na kodi ya nyumba inapanda.Vitegauchumi huingiza pesa bila kukulazimu kuendelea kufanya kazi hivyo hata ukizeeka au kuugua au kufukuzwa kazi vitegauchumi vyako vinaweza kukulinda kwani vitaendelea kukupa kuipato bila kufanya kazi. Swali la kujiuliza ni jee chanzo chako kikuu cha mapato yako ni katika kazi unazozifanya kila siku au kutoka kwenye vitegauchumi? Kama unategemea kazi kuingiza sehemu kubwa ya kipato chako una hatari ya siku moja kurudi kwenye umasikini kama ukiugua muda mrefu, kufukuzwa kazi au kustaafu.Jitahidi kuwekeza pesa zako kwenye vitegauchumi vilivyo endelevu ili uwe na uhakika wa maisha.
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;  http://mshauriwabiashara.weebly.com

Read More ...

0 comments


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara (mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya. Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara (Business idea) huanza kwanza kwa kuchunuguza fursa zilizopo katika eneo husika. Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan). Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo, naomba kuorodhesha baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji: 1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi? 2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi? 3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko vipi? 4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya kutosha? 5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila siku? 6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani? 7. ............................. 8. ............................. Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza kutokana na mazingira husika. Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika jamii kuwa ni kawaida, kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida, lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza wazo la biashara. Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo. Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua. Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi.
Read More ...

1 comments
Mawasiliano bora  ni muhimu sana kwa mafanikio yetu katika nyanja mbalimbali.  Kama hatuna mawasiliano yaliyobora au hatuwezi kuwasiliana inavyotakiwa basi itakuwa ngumu kwa watu wengine kutusaidia katika kile tunachokihitaji.  Mawasiliano yasiyo bora au kushindwa kuwasiliana vema kunadumaza na mara nyingine kuua  kabisa mahusiano baina yetu na wengine.  Kwa  maana hii basi hauna budi kuzingatia sana maelezo na ushauri kutoka katika mada hii na kuyaweka maelezo haya katika matendo ili yakusaidie maishani.
Vitu vya kuzingatia.
 1. Yatazame au yachukulie mazungumzo yako na wale unaohusiana nao kama majadiliano ya kawaida tu na sio mashindano.
Hii itakusaidia kuwa na mahusiano na mawasiliano bora na wengine hususani pale utakapoyaona yale mnayozungumza mara kwa mara kama majadiliano na siyo mashindano. Majadiliano ni mazungumzo yenye kusudi la kufikia suluhisho au muafaka fulani.  Ni mazungumzo ambayo yanapotumika nia yake siyo kumuumiza, kumuumbua mtu bali kutoa nafasi kwa pande zote kufikia matokeo bora. 
Mazungumzo ya yenye ushindani ni yale yenye nia ya kuumiza, kuumbua, kuaibisha, na kudharaulisha, na ambayo nia yake ni kumuonyesha mshindi na aliyeshindwa mwishoni mwa mazungumzo hayo.
Wale wenye tabia ya kuzungumza kiushindani huyachukulia mazungumzo kama nafasi ya kuonyesha ubabe au kunyanyasa wengine. Hata kama  yule mnayezungumza naye ana nia ya mashindano, wewe fanya majadiliano ya kawaida ili taratibu uweze kumbadilisha mtazamo wake.
 1. Kuwa msikilizaji makini na hitaji kusikilizwa pia
Kati ya alama za uonyesha kuwa wewe ni mwenye mawasiliano bora ni pamoja na uwezo wa kuwa msikilizaji mzuri.  Wako watu ambao hupenda kuongea tu na sio kusikiliza.  Sambamba na hilo, unatakiwa kuomba na wewe pia usikilizwe vizuri. Muombe yule anayekusikiliza akuache umalize kuongea ndio na yeye aanze kuongea.  Kamwe hamtafikia muafaka wowote ikiwa wote wawili mnaongea kwa wakati  mmoja.
Yafuatayo yatakuwezesha kuwa msikilizaji mzuri
-          Msikilize yule anaeongea kwanza na kumuelewa
-          Fahamu fika kile kinachozungumzwa elewa nia na dhumuni la majadiliano
-          Uliza swali pale unapodhani hujaelewa ili uweze kuelewa vema nia ya mzungumzaji
-          Jaribu kuweka kwa kifupi au kwa muhtasari kile kilichozungumzwa, mweleze anayezungumza unavyojihisi juu ya  alichokuwa akikieleza, na hakikisha  ulimuelewa vema.
-          Eleza unavyofikiri wewe.  Mweleze aliyekuwa anazungumza kama umekubaliana nae au la, toa sababu za kukubaliana au kutokukubaliana.
 1. Kuwa mzungumzaji mwenye ujasiri.
ujasiri katika mazungumzo huchochea uhalisi na kuaminika katika kile unachokisema.
Zifuatazo ni tabia za mzungumzaji bora;
a)      Tumia sentensi zinazokuelekea wewe zaidi ya sentensi zinazo waelekea wengine. Jilenge wewe zaidi ya kuwalenga wenzako unapozungumza. unapotumia sentensi za “ninyi” au “wewe” mara nyingi unaweza kuonekana usiye na ujasiri, tofauti na pale unapotumia sentensi zenye “mimi”. Unaweza kuonekana pia kama usiye yaamini  maneno yako.
      Sentensi zenye ujasiri na zenye kukulenga wewe binafsi ni kama vile
 “nimefurahi kukuona”
 “Ningependa kuzungumza na wewe”   
“Sijafurahishwa na maneno yako”
b)      Katika  mazungumzo yako tumia zaidi sentensi na siyo maswali. Hii itakuwezesha pia kuonyesha kuwa unaujasiri katika kile  unachokisema na unajiamini  wewe mwenyewe pia.
Mfano wa mazungumzo yakutumia swali: “Hivi ninyi mnamwonaje yule rafiki yetu?”
Badala yake  ungetekiwa kusema “mimi sifurahishwi na matendo ya huyu rafiki yetu”
Au maranyingine baba wa nyumba anapouliza “Hivi mnadhani nani baba humu ndani?” hii huonyesha kutojiamini kwake
“Hivi unafikiri mimi njinga?”
“Hivi jamani  sisi hatupewi huduma?”
Namna nyingine bora zaidi ya kuuliza swali
-          Je waweza kunisaidia tafadhali?
-          Je utakubali kuoana na mimi?
       Namna bora ya kuzungumza katika sentensi
-          nitafurahi sana ikiwa utakubali kuoana namimi.
-          Nitafurahi sana kupata msaada kutoka kwako
c)      Tumia zaidi sentensi zenye “kukiri” na sio sentensi zenye lawama. Sentensi zenye ukiri au kukiri ni zile ambazo anayezungumza anasema kile ambacho angetaka aone kikifanyika au kile ambacho angependa akione kikitendeka.
Kinyume chake ni sentensi zenye lawama; hizi ni zile ambazo mzungumzaji ana sema kile asichotaka, au kile asichokipenda kitokee au kifanyike.
Mfano wa sentensi zenye lawama:
·         Sipendi kabisa vile unavyonichukulia
·         Sipendi kabisa unavyoniingilia katika maongezi
Mfano wa sentesi zenye kukiri; “Ningefurahi kama ungesubiri nimalize kwanza kuongea  halafu na wewe utaongea”
Sentensi zenye lawama huonyesha ukosefu wa ujasiri kwa mzungumzaji,  mbaya zaidi, sentensi hizi hazisaidii chochote katika kubadili tabia ya yule anayeambiwa maana hazionyeshi bayana ni nini kinachotakiwa kufanyika.
Sentensi zenye lawama pia huonyesha wazi tabia yako sugu ya kulaumu, pia huonyesha vitu usivyovipenda tu, na kuvisahau vile vizuri unavyovipenda.  Ni ngumu sana kumsaidia mtu ambaye analaumu usiku na mchana kuwa hapendi hiki, hapendi kile, hataki hiki na wala hataki kile na bado hawezi kusema anapenda au kutaka nini badala yake.  Kwa hali hii watu hawa wanabaki kuwa walaumu mara dufu.
 1. Lugha ya  mwili wako iwe nzuri (Positive Body language)
Lugha ya mwili ni vile tunavyoweza kutumia miili yetu kuonyesha nia zetu.  Mwili ni kiungo muhimu sana cha mawasiliano.  Tafiti zinasema kwamba, hata wakati mtu anazungumza kupitia mdomo, asilimia 60 (sitini) ya ujumbe wake kupitia au kueleweka sio kwa kupitia maneno ya kinywani mwake bali ni kwa kupitia lugha ya mwili wake.  Jambo hili ndilo hutiliwa  mkazo na ule usemi usemao “matendo husungumza zaidi kuliko maneno”
Lugha ya mwili huusisha vitu kama vile; muonekano wa sura (facial impression), mikunjo ya uso, macho yalivyowekwa, kinywa kilivyo tumiwa, pua inavyofanywa wakati wa kuongea, mikono na pozi ya mwili ilivyo wakati wa kuzungumza.
Ni vema kujikumbusha kila wakati kuhusu umuhimu wa lugha ya mwili ili itusaidie kujijua sisi wenyewe na ule ujumbe tunaoutuma.
Hapa nataka kujaribu kueleza baadhi ya maeneo ya lugha ya mwili ambayo yatakusaidia kuweza kubadilika au kujirekebisha katika mchakato mzima wa mawasiliano kupitia mwili wako.
a)      Kutembea kwa hatua za kudunda au kunesa
Kutembea huku kuwasilisha hisia za ujasiri. Tabia hii huweza kuwa ya asili au ya kujifanyisha hususani apale unapodhani kuwa unachofanya ni cha muhimu zaidi na unapoamini kuwa wewe ni bora zaidi. Kutembea kwako kwaweza kuonyesha  kila kinachoendelea akilini mwako.
b)     Kupanda au kushuka, uzito au wepesi wa sauti unapoongea (Tone of voice)
Pale unapojua hauna ugomvi au uadui na yeyote basi sauti yako itakuwa nzuri, na yakiasi cha kusikika na yeyote.  Vituo vyako na misemo yako itakuwa ya kawaida na yenye uwiano. Pale unapohisi hofu, au kuwepo kwa wabaya wako, mara nyingi sauti yako huwa chini na isiyo na ujasiri.
Unashauriwa kwa hali yoyote ujitahidi kuzungumza kwa sauti ya kati, isiyo chini sana wala juu sana.
c)      Mavazi sahihi
Unapohisi una nafasi fulani katika jamii au sehemu fulani utajikuta unajali sana   suala la kuvaa kwako. Mavazi huweza kuzungumza nia ya moyo na huweza kuonyesha picha mbaya au nzuri kwa wanao kutazama. Mavazi ya aina fulani huweza kukupa tafsiri mbaya kwa watu tofauti na vile ulivyo kihalisia, au kwa upande mwingine mavazi mengine yamefanya wengine kuonekana kama vile ni wa maana sana na wakutegemewa wakati uhalisi haukuwa hivyo
d)     Pozi zuri la mwili
Kuketi au kutembea katika mwili ulionyooka huonyesha ujasiri.  Hii inamaana kifua kinakuwa mbele na tumbo ndani kidogo.  Hata askari waliojasiri huwa hulazimika kuwa katika pozi hili.  Pozi zuri ni ishara ya ukakamavu na afya njema pia.
e)      Muonekano wa macho
Muonekano wetu machoni huweza huonyesha hofu, aibu au ujasiri, hususani tunapokutwa katika maeneo au matukio ambayo hatukutarajia. Muonekano wa macho huthibitisha ukweli au uongo wa kile tunachozungumza.  Muonekano wa macho yetu huweza pia kuthibitisha kumaanisha au kutokumaanisha, uhakika au kutokuwa na uhakika katika kile tunachokizungumza. Wako wengine wasioweza kamwe kuwatazama machoni wale wanaowahofia au kuwaogopa. 
f)       Ukaribu au mgusano
Tabia ya kujitenga na wengine huweza kumaanisha kujikweza au kukosa ujasiri.  Jaribu kuwa karibu na wengine zaidi kadri utamaduni wa jamii uliyopo unavyokuruhusu.  Kama kukumbatia kunaruhusiwa katika jamii yako fanya hivo, kama kushika mkono ndio kunakoruhusiwa basi hakikisha unafanya hivyo, mara kwa mara. Mgusano wa mwili unamaana kubwa sana katika kuongeza ukaribu baina ya watu.
g)      Ishara za mwili (gestures)
Tumia ishara unapoongea. Mfano tumia mikono, tumia kichwa na macho kusisitiza unachoongea.  Kuongea tu kwa madomo pasipo kiungo chochote cha mwili, hufanya mazungumzo yako huwa butu sana.  Ishara za mwili tunazitumia kusisitiza au kuthibitisha tunachokiongea.  Ishara hizi za mwili zitumike taratibu, zisizidishwe sana maana na zaweza kuwabughudhi wengine.
Chris Mauki
Social, Relationship and Counseling Psychologist
E-mail: chrismauki57@gmail.com
Read More ...

0 comments

UJASIRIAMALI---UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

Idadi ya wanyama wanaofugwa kwa chakula imezidi ile ya binadamu zaidi ya mara mbili kote ulimwenguni. Kuna maelfu ya wanyama kote duniani ilihali ni wachache tu wanaoweza kufugwa. Kati ya hawa wanyama, ni aina nne (Ng'ombe, kondoo, mbuzi na kuku) wanaochukua asilimia 95% ya wanyama wote wanaofugwa. Wanyama hawa hupatikana katika nchi za hari kwenye nyanda za chini. Lakini kati ya mifugo hawa, kuku ni maarufu katika nchi za hari na hata kote ulimwenguni.Lengo la makala haya ni kutoa maelezo ili kusaidia wafugaji wa kiwango kidogo katika nchi
zinazostawi, katika kupunguza umaskini. Sehemu ya kwanza (I) itatoa maelezo kuhusu ufugaji na
hasa ufugaji wa kuku, Sehemu ya pili (II) itaangazia maswala yafuatayo katika kuinua hali ya uchumi
kwa kufuga kuku:
1. Kuendeleza ufugaji wa kuku za kienyeji kwa kutumia njia zisizohitaji gharama nyingi.
2. Kutafuta mbinu na njia muafaka za kuzalisha viwango vya kuku bora kwa njia ya kiasili.
3. Matumizi ya njia za kiasili au zile zisizo gharimu pesa nyingi kutibu na kuzuia magonjwa ya
kuku.
SEHEMU YA I: MAELEZO KUHUSU UFUGAJI WA KUKU KATIKA NCHI
ZINAZOENDELEA
NAFASI YA MIFUGO
Licha ya kukosa mashamba makubwa ya kuendeleza ufugaji wa ng'ombe, jamii nyingi katika nchi za
hari (tropics) hupata nafasi ya kufuga kuku kwa kiwango kidogo. Idadi ya wanyama wanaofugwa
huongezeka sambamba na ile ya watu. Idadi ya watu inapoongezeka ndipo ile ya mifugo huzidi.
Idadi kubwa ya watu huhitaji chakula kingi na matumizi huongezeka, hivyo basi watu hufanya bidii
kuzalisha chakula na mapato kutoka kwa shamba.
Ufugaji wa ng'ombe na wanyama wanaohitaji lishe kwa wingi huhitaji kiasi kikubwa cha shamba ili
kupanda mimea na lishe la mifugo. Ukilinganisha na ufugaji wa kuku, utahitaji mabaki ya vyakula
na sehemu ndogo ya shamba. Ufugaji wa kuku umeweza kunawiri hata pasipo fedha.
Katika nchi za hari ufugaji wa kienyeji hautahitaji kazi nyingi, kazi hii hufanywa na akina mama na
watoto. Kwa kawaida katika nchi hizi kazi nyingi za nyumbani hutekelezwa na mama. Vyakula vya
kuku vyaweza kutoka kwa: 1) Mabaki ya chakula, 2) Mabaki ya mimea, 3) Mabaki kutoka jikoni
na 4) Vyakula vya kujitafutia (kwa mfano kwekwe, mbegu, wadudu, nyongonyongo, n.k). Mfumo
wa kufuga kuku kwa njia ya kienyeji hutumia viungo vinavyopatikana kwa urahisi na kuimarisha hali
ya kiuchumi na chakula bora kwa jamii.
Ni muhimu sana kufuga mifugo hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo kwa sababu ya 1) Chakula bora
na kuongeza mapato ya jamii kwa viwango vya kuridhisha; 2) Mifugo ni hakiba au banki, faida yake
huzaana tu kama riba ya benki; 3) Mifugo yaweza kuuzwa ili kugharamia karo ya wanafunzi,
malipo ya hospitali, gharama nyingine za nyumbani na hata shambani; 4) Kwa matumizi ya kijamii
(kwa mfano kulipia mahari, shughuli za kidini, n.k); 5) Mifugo husaidia katika kukabili wadudu,
kwekwe na kuimarisha rutuba kutokana na mbolea ya kinyesi. Ni bayana kwamba mifugo ni
muhimu sana kwa mkulima yeyote yule.
UMUHIMU WA UFUGAJI WA NJIA YA KIENYEJI
Ufugaji wa kuku katika nchi zinazostawi waweza kugawanywa mara mbili: 1) Ufugaji wa
kitamaduni au kienyeji pasipo kuwepo gharama, na 2) Ufugaji wa kisasa unaohitaji fedha nyingi.
Ufugaji wa viwango vikubwa kwa kuzingatia mfumo wa kisasa ni maarufu katika kuzalisha kuku wa
nyama na wale wa mayai. Mfumo huu hujumuisha asilimia ndogo sana ya aina ya ufugaji.
Itafahamika kwamba mfumo wa kisasa haujaadhiri ule wa kienyeji. Idadi kubwa ya watu katika nchi
za hari hutegemea mfumo wa kienyeji kwa nyama na mayai.
Mfumo wa kisasa huhitaji pesa nyingi za kununua vyakula vya kuku. Aidha mfumo wa kisasa huhitaji kazi nyingi ili kutekeleza. Mfumo wa kisasa
umefaulu katika nchi zilizostawi kutokana na hali nzuri ya kiuchumi katika kuzalisha (kuku wa hali
ya juu, kuangua vifaranga kwa stima, vyakula vilivyo na madini mengi, vifaa na zana za mashine,
utaalamu wa hali ya juu n.k). Haitafaa sana kuanzisha mfumo kama huu katika vijiji vya mataifa
yanayostawi.
"Mageuzi" katika ufugaji (kuambatanisha mfumo wa kisasa pamoja na ule wa kienyeji) yamefanyiwa
majaribio katika mataifa yanayostawi tangu miaka ya 1950. Matokeo ya kuku wapatao 200 hadi 300
kwa shamba moja hayajawai kufaulu. Hasara imepatikana na waweza kuona nyumba zilizokuwa na
kuku bila chochote, pesa nyingi zimepotea na kuku hawapo.
Mfumo wa kienyeji ni bora (Katika hali ya kiuchumi) iwapo idadi ya kuku haitazidi kuku 50. Ni
rahisi kuweza kuwatunza kuku, kwani hakuna gharama nyingi. Iwapo vyakula au zana za kisasa
zitanunuliwa, basi haitakuwa kwa viwango vikubwa. Mazao ya nyama na mayai yataleta faida.
Sehemu nyingi katika mataifa yanayostawi hakuna stima, katika nchi za hari, ufugaji kwa kiwango
kidogo umeweza kufaulu na kuimarisha uchumi.
FAIDA ZA UFUGAJI WA KUKU KWA NJIA YA KIENYEJI
Faida za uzalishaji kuku ili kuimarisha uchumi kwa njia hii zimepuuzwa na viongozi na wafadhili.
Kuku huleta faida kwa jamii kama tulivyoona katika sehemu ya I. Zaidi ya hayo, ufugaji wa kuku waweza kuimarishwa pasipo gharama nyingi ukilinganisha na mifugo wengine.
· Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai
· Mayai ni chakula kilicho na madini muhimu na kisicho ghali katika soko lolote. (madini kama methionine na cystine), madini haya ni muhimu sana kwa afya ya watu hasa watoto wachanga. Pia hutupatia protini.
· Kinyesi cha kuku ni mbolea safi
· Kiwanda asilia cha kutotoa vifaranga
· Gharama za kuanzisha na kuendeleza ni nyepesi
· Kitoweo chepesi na rahisi kwa wageni, kitoweo hakihitaji hifadhi hutumika mlo mmoja au miwili na kumalizika
· Jogoo hutumika kama saa inapowika
· Manyoya ya kuku hutumika kutengenezwa mapambo mbalimbali, mito na magodoro
· Kuku wanahisimu wadudu waharibifu
Kuku ndiye mnyama wa kipekee anayeweza kuishi mahali popote hapa ulimwenguni bila kuadhiriwa
na viwango vya hali ya hewa. Ufugaji wa kuku ndio shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji wa aina yeyote. Kuku hunawiri vyema katika nchi za hari kutokana na uwiano uliopatikana wakati wa mwanzo binadamu alipofuga Asian jungle fowl aina ya kuku-mwitu. Mayai pia yaweza kuhifadhiwa kwa urahisi na huchukua nafasi ndogo kuliko aina ya bidhaa zozote za mifugo. Mayai yaweza kuwekwa mahali kwa muda mrefu bila kuhitaji barafu. Hautahitaji kuhifadhi kuku kwa njia yoyote, kwani nyama yake hupatikana pale unapohitaji kwa kuchinja.
Upungufu wa kuku wa kigeni ukilinganisha na wale wa kienyeji ni kama ufuatao:
• Kuku wa kigeni hawawezi kukalia na kuangua mayai, hivyo basi wahitajika kununua vifaranga (gharama);
• Vifaranga wa kigeni huhitaji utunzaji maalum na vyakula maalum (gharama);
• Kuku waliozalishwa kwa njia ya kisasa huhitaji chakula kingi ili kutaga mayai (gharama);
• Kuku wa kisasa huhitaji zaidi kuchanjwa dhidi ya magonjwa (gharama)ukilinganisha na wa kienyeji (japo nao huhitaji chanjo);
• Kuku wa kutaga mayai huhitaji mwangaza wa stima (saa 14 kwa siku) ili kutaga mayai (gharama)
Kwa kuongezea, rangi ya nyama na mayai ya kuku wa kienyeji huvutia kuliko ile ya kuku wa kisasa.
Hivyo basi jaribu kuendeleza na kuhimiza ufugaji wa kuku za kienyeji.
Iwapo mkulima ana jogoo mmoja na kuku kumi na mbili, basi kila mwezi waweza kupata kuku
akikalia mayai 10-12 kwa mwezi (mayai yote kwa wakati mwingi hayataanguliwa) kuna hakikisho la
kupata vifaranga vinne kila mwezi. Kuku mzima atachukua miezi minne kuchunga vifaranga
walioanguliwa. Kwa hivyo, kati ya kuku wote kumi na mbili kila mara kutakuwa na kuku wanne
wakitunza vifaranga, huku wale wengine wanane wakitaga mayai.
Kuku waliofugwa kwa njia ya kitamaduni hupata vyakula vyao kwa kutafuta mbegu, wadudu
nyongonyongo, n.k; Lakini kuku hawa hukosa vyakula vya kutosha vilivyo na nguvu ili waweze
kutaga mayai. Vyakula vya kutoa nguvu daima huwa ni haba.
Waweza kuwalisha kuku kwa nafaka ili wapate chakula cha nguvu (mfano kilo moja ya nafaka
iliyopondwa kila siku kwa kuku 10), nafaka hii yapaswa kuwa kavu. Vifaranga wapewe kiasi kidogo
cha nafaka au mchele wiki za kwanza. Kuku wanaolishwa nafaka baada ya kujitafutia chakula nje
huongeza idadi ya mayai (kutoka asilimia 20-25% hadi 40-50%). Kuna umuhimu wa kuhifadhi
nafaka kama lishe badala ya kuuza kwani utapata mayai mengi ambayo baadaye utaweza kuuza.
Hautahitaji kununua vyakula vya protini kwani kuku hujitafutia lishe la protini.
Ikiwa hauna nafaka, waweza kutumia vyakula vya mzizi au ndizi. Vyakula vya aina hii hata hivyo,
huwatatiza kuku wanapovitonogoa, kiwango cha mayai sio kikubwa kama cha wale wanaolishwa
nafaka.
Kwa kuwalisha kuku kwa nafaka utapata hakikisho la mayai manne kwa siku kutoka kwa wale kuku
wanane. Iwapo hakuna nafaka, kati ya kuku wanane wanaotaga utapata mayai mawili tu kwa siku.
Ni bora kutumia nafaka hii kama lishe kuliko kuuza na hatimaye kununua vyakula vya dukani.
Kuku kumi na mbili na jogoo mmoja wanaolishwa kwa kilo moja ya nafaka kila siku waweza
kuelezwa hivi:
• Waweza kuuza kuku wanne kila mwezi na kujaza pengo hilo na wale vifaranga (vifaranga
wanne huanguliwa kila mwezi) na
• Dazani kumi za mayai kila mwezi (mayai manne kila siku).
Kwa mwaka mmoja waweza kukadiri ile faida utakayopata na vile hali ya kiuchumi yaweza
kuinuliwa katika mataifa yanayostawi.
Hata hivyo faida hii haitaafikiwa iwapo magonjwa
hayatazuiwa au kukabiliwa kama ifuatavyo.
TEKELEZA UTARATIBU WA KUZUIA MAGONJWA
Magonjwa ndio husababisha hasara katika mfumo wa ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya
magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko
kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu) dhidi ya magonjwa
yafuatayo:
Ugonjwa wa Newcastle
Ugonjwa huu ndio huadhiri kuku na kusababisha hasara katika nchi za hari. Virusi vya ugonjwa huu
huenea kwa kasi na rahisi kiasi cha kusababisha vifo kwa asilimia 100%. Dalili za kwanza ni shida
ya kupumua na kung'amua hewa, sauti kama ya kikohozi na kutokwa mate. Kinyesi chaweza kuwa
na rangi ya kijani kibichi. Hadi sasa hakuna dawa.
Waweza kuzuia ugonjwa huu kwa kutoa chanjo. Dawa za chanjo hupatikana kote ulimwenguni hata
katika nchi za hari kwenye vipimo vya vitone mia moja. Madawa haya yaweza kuhifadhiwa kwa
muda. Waweza kuweka kwa wiki moja mbali na jua au joto kali (Chanjo hii ni ya kipekee, kwani
aina nyingine ya chanjo huwekwa kwa friji). Waweza kutoa chanjo kwa kutia vitone kwenye
mdomo. Kuku wote (wakubwa kwa wadogo) wapaswa kupewa chanjo baada ya kila miezi mitatu.
Minyoo
Minyoo kama chango (roundworms) na tegu (tapeworms) huadhiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya chakula, mayai hupungua na magonjwa mengine hushambulia. Ni bora basi kutoa minyoo.
Mchanganyiko wa madawa ya aina tatu ndio hutumiwa kuangamiza minyoo, madawa haya ni
piperazine, phenothiazine na butynorate. Madawa haya hupatikana kama vidonge (tumia kidonge 1
kwa kuku mzima na 1/2 kwa vifaranga). Iwapo hautapata dawa hii, waweza kutumia Panacur au
dawa nyingine ya kuangamiza minyoo. Wapatie kuku dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.
Wadudu
Wadudu kama chawa au utitiri husumbua kuku katika ufugaji wa kienyeji. Chawa au utitiri
husababisha harara ya ngozi, kuku walio adhiriwa hupata shida na kukosa usingizi. Hali hii
hupunguza kiwango cha mayai na uzito wa kuku.
Tumia asilimia 5% ya unga wa malathion kwa kupulizia kuku (puliza kwa chupa uliyo toboa
mashimo) pulizia kila kuku ili kuzuia chawa na utitiri (kilo moja ya unga huu yaweza kutibu kuku
150). Pulizia dawa hii baada ya kila miezi mitatu, waweza kupuliza kwa wakati mmoja wa kutoa
chanjo na dawa zilizotajwa hapo juu. Puliza unga huu pia kwenye viota vya kuangulia mayai.
Waweza kutayarisha 5% ya malathion kwa kuchanganya 25% ya unga wa malathion (kiwango cha
kilimo) na sehemu nne za jivu kutoka jikoni.
Magonjwa ya mapafu
Magonjwa ya mapafu huadhiri njia inayopitisha hewa na kuambatanisha mate na sauti kama ya
kikohozi. Ugonjwa huu huenea polepole. Uambukizanaji pia hutokea kwa polepole na vifo sio kwa
wingi. Hata hivyo, kutaga mayai na uzito hupungua. Shida hii yaweza kusambaa hata kutoka mahali vifaranga huanguliwa hadi pale walipouzwa.
Tylosin19 ndio dawa inayoweza kutibu magonjwa ya mapafu. Kiasi cha 35mg ya tylosin hutosha
kuku mmoja (kiwango hiki hufaa kuku na hata vifaranga) dawa hii husimamisha madhara kutokana
na magonjwa ya mapafu. Tibu kuku kila baada ya miezi mitatu, waweza kutekeleza kwa wakati
mmoja wa kutoa kinga na kuangamiza minyoo. Tylosin hupatikana kwa pakiti ndogo ya 4gm.
Waweza kutayarisha dawa hii kwa kutumia maji na 35gm ya tylosin (gramu nne kwa vikombe viwili
vya maji), kiasi hiki chaweza kutolewa kwa vitone kwa kila kuku.
.............................. ....//.............................. .
KWA UFUPI (SUMMARY)
Kabila za Kuku
Si rahisi kupata kabila halisi (pure breed) au kizazi halisi (pure line) za kuku wa kienyeji kutokana na mwingiliano wa vizazi kati ya aina mbalimbali za kuku hao. Lakini hata hivyo baadhi ya kuku wa kienyeji wanaweza kutambuliwa kutokana na maumbile yao kwa mfano
1. Kuchi
 • Warefuna wenye kusimama mgongo ukiwa wima
 • Wana manyoya machache mwilini na vilemba vyao ni vidogo
 • Majogoo huwa na wastani wa kilo 2.5 na mitetea kilo 1.8
 • Mayai gram 45

2. Ching'wekwe (Umbo dogo)

 • Hupatikana zaidi Morogoro na umasaini
 • Majogoo kilo 1.6
 • Mitetea kilo 1.2
 • Yai gram 37
 • kuku hawa wanafaa sana kwa biashara ya mayai kwa kuwa hutaga mayai mengi sana.

3. Umbo la Kati

 • Majogoo kilo 1.9
 • Mitetea kilo 1.1
 • Mayai gramu 43
 • Hukua upesi na hupata kinga upesi baada ya kuwachanja dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle)

4. Singamagazi

 • Hupatikana zaidi Tabora
 • Majogoo wana rangi ya moto na mitetea rangi ya nyuki
 • Majogoo kilo 2.9
 • Mitetea kilo 2
 • Mayai gramu 56

5. Mbeya

 • Wanapatikana Ileje Mbeya na asili yao ni Malawi
 • Mjogoo kilo 3
 • Mitetea kilo 2
 • Mayai gramu 49
 • Uwezo wao wa kuatamia mayai na kuangua ni mdogo sana ukilinganisha na kuku wengine

6. Pemba

 • Maumbo ya wastani na miili myembamba
 • majogoo kilo 1.5
 • mitetea kilo 1
 • mayai gramu 42

7. Unguja

 • Hawatofautiani sana na wa Pemba
 • Vilemba vyake ni mchanganyiko- vidogo an vikubwa
 • Majogoo kilo 1.6
 • Mitetea kilo 1.2
 • Mayai gramu 42

SIFA WA KUKU WA KIENYEJI

 1. Wastahimilivu wa Magonjwa
 2. Wana uwezo wa kujitafutia chakula
 3. Huatamia, kutotoa na kulea vifaranga
 4. Wanastahimili mazingira magumu(ukame, baridi n.k)
 5. Nyama yake ina ladha nzuri

KATIKA KUWAENDELEZA KUKU WA KIENYEJI NI VYEMA

 1. Wajengewe nyumba bora
 2. Wapewe kinga dhidi ya ugonjwa wa Mdondo (New Castle), Ndui (Fowl Pox) pamoja na kinga ya minyoo.
 3. Malezi bora ya vifaranga
 4. Kuwapatia chakula cha ziada pamoja na maji ya kunywa ya kutosha.

NYUMBA BORA
Eneo inapojengwa nyumba au banda la kuku liwe

 • Linafikika kwa urahisi
 • Limeinuka juu pasituame maji
 • Pasiwe na pepo zinazovuma

Vifaa kama miti, nyasi, makuti, fito, udongo mabanzi ya miti, cement, mabati n.k
Sifa za Nyumba Bora ya Kuku

 • Paa imara lisilovuja
 • Kuta zisiwe na nyufa
 • Sakafu isiwe na nyufa
 • Madirisha ya kutosha kupitisha hewa
 • Iwe na mlango wa kuingia kufanya usafi
 • Iwe na ukubwa (nafasi) unaolingana na idadi ya kuku. Wastani wa kuku 10-15 kwa mita moja mraba

Mambo muhimu ndani ya nyumba

 • Chaga za kulalia kuku
 • Sakafu iwekwe maranda (wood shavings), makapi ya mpunga, n.k
 • Viota vya kutagia mayai sentimita 35x35x35 na idadi ya viota iwe nusu ya idadi ya kuku waliofikia hatua ya kutaga na viwekwe sehemu iliyojificha (faragha)

UATAMIAJI WA MAYAI
Kuna njia 2

 • Njia ya kubuni (incubators)
 • Asili

Kumuandaa kuku anayeatamia

 • Weka maranda au majani makavu ndani ya kiota
 • Anapokaribia kuatamia toa mayai ndani ya kiota pamoja na maranda, hakikisha mikono haina manukato
 • Nyunyiza dawa ya kuua wadudu (viroboto, utitiri n.k) ndani ya kiota, pia mnyunyizie dawa kuku anayetarajia kulalia mayai
 • Rudisha mayai kwenye kiota ili kuku aanze kuatamia
 • Kwa kawaida kuku hulalia mayai yake kwa muda wa siku 21 ndipo huanguliwa

ULEAJI WA VIFARANGA
Kuna njia mbili

 • Njia ya kubuni
 • Njia ya asili

Njia ya ASILI
Kuku mwenyewe hutembea na vifaranga akivisaidia kutafuta chakula. Ni vizuri kumtenga kuku mwenye vifaranga katika chumba chake pekee ili vifaranga wasishambuliwe na kuku wengine hali kadhalika kuwalinda na wanyama na ndege wanaoshambulia vifaranga.
Njia ya KUBUNI
Vifaranga huwekwa kwa pamoja kwenye chumba maalum na kupatiwa joto maalum, chakula pamoja na maji. Tumia taa ya kandili (chemli), umeme au jiko la mkaa na hiyo taa iweke kwenye mzingo(mduara) walipo vifaranga. Pia kuna kifaa kinaitwa Kinondoni Brooder ni kizuri kwa kutunzia vifaranga. Kwa kutumia kifaa hiki kuku wanaweza kunyang'anywa vifaranga vyao mara tu baada ya kutotoa na kuviweka kwenye hii brooder na hao kuku wakaachwa bila vifaranga vyao, baada ya majuma matatu au manne, kuku hao huanza tena utagaji na kuendelea na uatamiaji hadi kutotoa tena. Kwa mtindo huu kuku anaweza kutotoa mara 5-6 badala ya kama ilivyo sasa mara 2-3 kwa mwaka. Vifaranga vikae ndani ya brooder majuma 3-4 na baadaye fungua milango ya brooder kuruhusu vifaranga vitoke na kuzungukazunguka chumbani bila kuvitoa nje kw kipindi cha mwezi mmoja au zaidi kutegemeana na mazingira.
KULISHA KUKU WA KIENYEJI
Kuku mkubwa huhitaji gramu 120 za chakula kwa siku, ni vizuri kuku wanaofugwa huria (free range) kupatiwa chakula cha ziada gramu 30 kila siku nyakati za jioni.
Kuku walishwe

 • Mizizi-mihogo, viazi vitamu, mbatata, magimbi, n.k
 • Nafaka-mahindi, Mpunga, Mtama, Ulezi na Pumba za nafaka zote
 • Mboga-Mikundekunde, nyanya, milonge, majani ya mapapai
 • Matunda-Mapapai, maembe, n.k
 • Mbegu za Mafuta-Karanga, ufuta, mashudu ya pamba, alizeti, n.k
 • Unga wa dagaa
 • Maji

KUCHANGANYA CHAKULA CHA KUKU

 • Pumba.............kilo20
 • Mashudu ya Pamba n.k...kilo 3
 • Dagaa iliyosagwa.........kilo 1
 • Unga wa majani uliokaushwa kivulini na kusagwa........kilo 2
 • Unga wa Mifupa ..........kilo 0.25
 • Chokaa ya mifugo ........kilo 0.25
 • Chumvi........................ gramu 30
 • Vichanganyio/Premix...gramu 25

KUPANDISHA

 • Uwiano wa mitetea na jogoo ni mitetea 10-12 kwa jogoo mmoja
 • Sifa za mtetea ni mkubwa kiumbo, mtagaji mayai mengi, muatamiaji mzuri na mlezi wa vifaranga
 • Sifa za jogoo ni awe mkubwa kiumbo, miguru imara na yenye nguvu, mrefu, upanga/kilemba kikubwa, awe na uwezo wa kuitia chakula mitetea na awe na tabia ya kupenda vifaranga
 • Jogoo huanza kupanda akiwa na umri wa miezi 7-10 na kuendelea hadi miaka mitatu na asipande watoto wake
 • Mitetea huanza kutaga wakiwa na miezi 6-8

MAGONJWA YA KUKU
1. Mdondo/New castle
Virus vinavyosababisha ugonjwa huu huenezwa kwa hewa
Dalili

 • Kuhalisha choo cha kijani na njano
 • Kukohoa na kupumua kwa shida
 • Kupinda shingo kwa nyuma
 • Kuficha kichwa katikati ya miguu
 • Kukosa hamu ya kula na kunywa
 • Idadi kubwa ya vifo hadi 90%

Kinga

 • Chanjo (New Castle vaccine) kwa mpango wa siku 3, wiki 3, miezi 3
 • Epuka kuingiza kuku wageni
 • Choma au fukie mizoga ya kuku waliokufa kwa ugonjwa
 • Zingatia usafi wa mazingira

NDUIYA KUKU/ FOWL POX
Virus huambukizwa kupitia jeraha au mbu
Dalili

 • Vidonda vyenye utando wa kahawia/purple kwenye sehemu zinazoonekana
 • Kukosa hamu ya kula
 • Vifo vingi

Kinga

 • Chanja vifaranga wanapofikia mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya Fowl pox vaccine
 • Epuka kuingiza kuku wageni
 • Zingatia usafi wa mazingira

HOMA YA MATUMBO/FOWL TYPHOID

 • Kuharisha kinyesi cha kijani na nyeupe
 • Kuku hukosa hamu ya kula
 • Kuku hukonda
 • Vifo hutokea kidogo kidogo kwa muda mrefu
 • Kinyeshi hushikamana na manyoya

Tiba
Dawa aina ya antibiotic, sulfa na vitamini
Kinga

 • Usafi
 • Fukia mizoga
 • Usiingize kuku wageni
 • Chinja kuku wote mara ugonjwa huu ukiingia na safisha banda, pia pumzika kufuga kwa miezi 6

MAFUA YA KUKU/INFECTIOUS CORYZA
Hutokana na bakitelia na hushambulia hasa kuku wakubwa
Dalili

 • Kuvimba uso
 • Kamasizilizochanganyikana na usaha unaonuka
 • Macho huvimba na kutoa machozi na pengine upofu
 • Hukosa hamu ya kula
 • Mbawa huchafuka na kutoa harufu mbaya

Tiba
Dawa za Antibiotic, sulfa na vitamini
KUHALISHA DAMU/COCCIDIOSIS
Husababishwa na vijidudu vya Protozoa
Dalili

 • Kuharisha damu
 • Manyoya husimama
 • Hulala na kukosa hamu ya kula

MINYOO
Dalili

 • Kunya minyoo
 • Hukosa hamu ya kula
 • Hukonda au kudumaa
 • Wakati mwingine hukohoa

Tiba
Dawa ya minyoo/Pipeazine citrate kila baada ya miezi mitatu
WADUDU
Viroboto, chawa, utitiri
Dalili

 • Kujikuna na kujikung'uta
 • Manyoya kuwa hafifu
 • Rangi ya upanga kuwa hafifu
 • Ngozi kuwa nene, ngumu na yenye magamba yanayodondoka kama unga

Kuzuia

 • Ziba mipasuko sakafuni na kwenye kuta za banda
 • Fagia banda mara mbili kwa wiki
 • Nyunyiza majivu au chokaa mara moja kwa wiki mara baada ya kufagia
 • Choma masalia ya mayai yaliyoanguliwa
 • Nyunyiza dawa kwenye viota
 • Weka maranda, majani makavu, makapi ya mpunga ya kutosha sakafuni ndani ya banda la kuku
 • Fuata kanuni za chanjo
 • Tenga kuku wagonjwa wakae mbali na kuku wazima

UPUNGUFU WA VIINI LISHE KWENYE CHAKULA
Dalili

 • Kuku hupungua damu, uzito na kudumaa
 • Mifupa huwa laini na kutokuwa imara
 • Hutaga mayai yenye gamba laini na madogo
 • Huwa na manyoya dhaifu,
Read More ...

0 comments


Baada ya kukupa Tip#2 kwamba kila kijana anapaswa kuelewa umuhimu wa Kujithamini (Self-esteem) na Kujiamini (Confidence) na kuwa mambo haya mawili yanaweza kumjenga na kumbomoa mtu. Ukosefu wa kujithamini na kujiamini ndo mwanzo wa kuporomoka kwa mafanikio yako, tulikudokeza mbinu ya kuanzia ni kujiwekea nafsi yako katika mtazamo wa juu (positive self-talk).

Sauti inayosikikia ndani ya kichwa chako ina uwezo wa kukufanya ujithamini kwa hali ya juu katika kila hatua unayochukua kwenye mambo yako. Watu maarufu na wenye mafanikio kimataifa, mfano Oprah, Jay Z, Usain Bolt, Patrick Ngowi na wengine wengi wamekiri kuwa wanayo tabia ya ‘positive self-talk’ kwa muda mrefu sana.

Watu wenye mtazamo HASI hawaachi kulalamika hovyo, kila kitu wao hukichukulia negative. Ni wagumu kuji ‘adapt’ na hali halisi, hawana subira na hupenda kuponda kila mtu au kila kitu. Muda wao mwingi hupoteza katika kuwaza mambo yasiyoweza kuwasaidia chochote. Mara nyingi hujiangusha wenyewe kwa kuwa na mtazamo HASI na tabia ya ‘negative self-talk’. Tuangalie mambo yanayoendelea kichwani mwako, kama wewe ni katika kundi la watu wasiojiamini wala kujithamini;

- Una imani kuwa wewe hauko sawa kama mtu wa kawaida

- Unajisikia hovyo, mpweke na stress zimekujaa ndani yako

- Unajiona una mapungufu mengi mfano, mtu akikusifia “umependeza”, badala ya kusema “asante”, huku ukitabasamu, jibu lako huwa “aaah kupendeza nitapendeza mie bwana, nguo yenyewe mtumba na sura yenyewe hii kama…...”

- Unajiona kuwa thamani yako ni ndogo, mfano “mimi sifai”, “mimi mjinga – sina akili”, “kila mara nashindwa au nafeli”.

- Una mtazamo hasi juu yako binafsi na uwezo wako wa kutimiza malengo uliyojipangia, mfano –“sidhani kama nitaweza kufanikiwa hilo….” “Mimi siwezi bwana….” “Aaaah hiyo haiwezekani, haiwezi kufanya kazi”.

- Unapoteza kujiamini kwako na unaona ‘future’ ya mbele hakuna kitakachobadilika

- Una imani ndogo sana kwa vitu vilivyoko maishani mwako

- Una amini kuwa ulimwengu hauwezi kukutimizia mahitaji yako binafsi

- Una acha kujishughulisha katika kuhangaika kutimiza ndoto zako

- Unagundua kuwa huna furaha wala mafanikio kama watu wengine walio fanikiwa

- Unaona watu wengine kuwa ni bora zaidi, wenye nguvu na wana mafanikio kuliko wewe. Unawaacha wakutumie au wakusaidie mambo yako

- Unaumia chinichini, unasononeka au unasikitishwa na hao watu

- Unajiona wa hovyo, au usiye kuwa na shukrani kuwa na mawazo ya hivyo kwa hao watu

- Unajisemesha mwenyewe na kujinyamazisha. Unajiadhibu kwa kushindwa kuwa kama wengine

- Unapojitazama, unajiona kama unatumiwa na wengine ili wajinufaishe mahitaji yao

- Unajijengea kichwani mwako imani ya nguvu zaidi kuwa wewe sio mtu sawa, tena una kasoro

- Unaachana kabisa na swala zima la kujithamini na kila kukicha mambo hayo hapo juu yanajirudia upya tena na tena

Tuangalie sasa hii tabia ya kutokujithamini (negative self-talk) ina anzaje anzaje!

- Kuna baadhi ya matukio yaliyokukuta maishani mwako yanaweza kuwa chanzo cha kukuletea hali ya kutokujithamini (low self-esteem) katika maisha yako.

- Kushushwa thamani mara nyingi na kudhalilishwa – hii inaweza kutokea nyumbani, kazini, shuleni, au popote pale

- Kubeba lawama ya vitu ambavyo hujahusika wala sio kosa lako

- Kukosekana kwa kutimiziwa mahitaji yako ya msingi

- Kudhalilishwa au kuteswa, mfano mtoto kutukanwa sana au kupigwa hovyo

- Kufanyiwa udhalilishaji au mateso ya aina nyingine, mfano kubakwa au kubaguliwa

- Kuwa na "label" iliyogandishwa kwako na watu wengine, mfano mlemavu au kuambiwa una wazimu na akili zako haziko sawa

- Kupata ujumbe wa mara kwa mara kuhusu nini wazazi, walimu, n.k.. wanategemea kutoka kwako – hili linaweza kuwa tatizo zito sana kwa watu ambao mzazi wake ni mlevi

- Vitu vinavyo onyeshwa kwenye TV, Movie na matangazo ya biashara yanayo onyesha ni kitu gani kinachotarajiwa kutoka kwako na unatakiwa uwe vipi, kimaumbilie, kimavazi na kazi nzuri yenye status

Hivi ni baadhi tu ya vitu hatuwezi kuviorodhesha vyote ambavyo vina nguvu kubwa sana katika kukubomoa ‘self-esteem’ yako. Hivi vitu vinachangia katika kushusha thamani ya mtu na sio kosa lako. Vinaweza kuwa ni mambo mtu mwingine amekufanyia au jinsi mambo yalivyo katika mazingira unayoishi au uliyokulia.

Huna uwezo wa kumbadilisha mtu. Ila unao uwezo mkubwa wa kujilea, kujitunza, kujibembeleza, kujidekeza, kujipenda na kujipongeza mwenyewe na nafsi yako. Kizuri zaidi ni kuwa unayo ‘control’ KUBWA sana katika kucheza na fikra zako, mtazamo wako ndio silaha kubwa sana ya kukujenga, jinsi utakavyo ‘think’, kujisikia na kufanya kwenye maisha yako. Anza leo KUFUTA fikra zote mbaya (hasi) kichwani mwako, jaza positive things na utaanza kuona hali ya maisha yako inavyobadilika.

Tembelea ukurasa wetu kesho tukijaaliwa tutazungumzia jinsi utakavyo jikuta kwenye dimbwi la moto kama utashindwa kuachana na ‘negative thoughts’. Amini usiamini, mitizamo HASI na mambo yanayosikika kichwani mwako ni hali inayoweza kukubomoa. Tutakupa mbinu zingine zitakazokusaidia katika kujijengea tabia za kujiamini na kuachana na mawazo HASI ya kujishusha thamani. Tunakutakia siku njema!

kwa hisani y shear illusion
Read More ...

0 comments


Mada iliyopita tulikupa Tip#1 iliyoeleza kwa kifupi kuwa ili kijana awe na mafanikio kwenye masomo na maisha yake kiujumla, anapaswa kuelewa umuhimu wa Kujithamini (Self-esteem) na Kujiamini (Confidence) na kuwa mambo haya mawili yanaweza kumjenga na kumbomoa mtu.

Leo tunaanza kwa kuelezea umuhimu wa kujisemesha wewe binafsi katika mtazamo wa kuwa mambo ni shwari, mara zote elekeza mawazo yako kuwa mambo yataenda CHANYA (positive self-talk). Kujithamini kwa hali ya juu (high self-esteem) kunaweza kumsaidia mtu ajisikie vizuri binafsi na ulimwengu uliomzunguka. Mtu kuwa na mtazamo wa kujithamini kwa hali ya juu kunamaanisha yafuatayo;

- Unaamini kuwa wewe ni mtu sawa – ukiwa macho au umelala

- Ndani ya mawazo yako unajisikia umerelax na unaheshimu misingi yako

- Una imani nzuri kuhusu wewe binafsi na malengo unayoweza kuyafikia

- Unahisi kujiamini, na maisha yako ya baadae yanaonekana kuwa na muelekeo mzuri

- Una imani na mambo yaliyopo kwenye maisha yako

- Unaamini kuwa dunia ina uwezo wa kukufikisha kwenye mahitaji na ndoto zako

- Unakuwa na mshawasha kuhusu vitu, ideas ulizonazo, na unavifanyia kazi kwa vitendo

- Unajisikia fahari, umeridhika na mwenye furaha unapofanikisha malengo yako uliyojiwekea

- Unajua kuwa unao uwezo binafsi kufanya mambo unayopenda katika maisha yako

- Unawaza njia za ubunifu za kukufikisha kwenye mambo unayotaka pale unapopata vipingamizi

- Unayaona na kuyathamini mafanikio yako
Hayo hapo juu ni mitazamo wa mtu anaye jithamini kwa hali ya juu – sauti inayosikikia ndani ya kichwa cha mtu huyo. Unao uwezo wa kukaribisha hali ya kujithamini kwa hali ya juu katika maisha yako.

Mtu mwenye kujithamini kwa hali ya juu anaweza kujiletea mambo mengine pia kwenye maisha yake.
- hali ya utulimu moyoni na maishani mwake
- hali ya kujiangalia na kujitunza
- kuwa na mtizamo chanya (positive attitude) na kuwa na maisha yaliyojaa furaha
- muwazi, mcheshi na uwezo wa kujieleza
- hali ya kujitegemea na kuwa muwajibikazi
- nia ya kujichanganya na watu wa kila hali na maelewano mazuri
- uwezo wa kujiendeleza binafsi mara kwa mara

Kuweza kujithamini kwa hail ya juu ni njia kubwa katika kukusaidia kwenye maisha yako. Inaweza pia kuwasaidia wengine walio karibu na wewe kujisikia na amani, wame relax, wanathaminiwa na kuwa na motisha wakiwa karibu na wewe. Baadhi ya tafiti zimethibitisha kuwa unaweza kufanikiwa kuwa mwanamichezo bora kwa kufanya mazoezi ya kujisemesha ndani mwako mambo chanya (positive self-talk).

Hebu anza hilo jaribio leo. Anza kujiambia wewe ni kijana mzuri, huna presha na mtu, hupendi beef na mtu, utafanikiwa tu kwa nguvu zake Mwenyezi Mungu, kwani wao wameweza wana nini hadi wewe ushindwe?
Tembelea ukurasa wetu kesho tukijaaliwa tutazungumzia watu wenye mitizamo HASI na mambo yanayosikika kichwani mwao na hali hii inavyoweza kumbomoa mtu. Tutakupa mbinu zingine zitakazokusaidia katika kujijengea tabia za kujiamini na kuachana na mawazo HASI ya kujishusha thamani. Tunakutakia siku njema!

source :shear illusion
Read More ...

0 comments

Kuna mambo muhimu na misingi bora ambayo kila kijana anapaswa kuyajua ili awe na mafanikio kwenye masomo na maisha yake kiujumla. Haya mambo ya mtu kujithamini (Self-esteem) na kujiamini (Self-confidence) yanaweza kumjenga mtu na usipoyatilia maanani yanaweza kumbomoa mtu. Leo tutaanza kwa ufupi kuelezea mada yetu umuhimu wa kuwa na mtazamo chanya wa kujijenga. Ukifuata Tips zote 5 tutakazo kudondolea, utakuwa kwenye ngazi ya kuelekea kwenye mafanikio ya hali ya juu. Umeshawahi kusikia mara nyingi watu wakisema “huyo hajithamini wala hajiamini”, lakini je, unajua maana ya maneno hayo?

Jinsi unavyo jithamini ni jinsi gani unavyo pima thamani ya utu wako. Kuna siku ambazo unaweza kuamka ari yako iko juu na unajisikia poa sana, unakuwa mwingi wa furaha, na unaamini kuwa ndoto zako zote zinaelekea unakotaka, maisha yako unayapa thamani na maana zaidi. Na mara NYINGI au chache kuna siku ambazo unaamka hujisikii vizuri kabisa, huna amani moyoni, huna furaha, tena una mashaka na kila ukifanyacho na kuona utu wako hauna thamani.

Kuna baadhi ya watu huwa na tabia ya kukosa ari (kujishusha) kila wakati, wao hujiona hawana thamani yeyote, hata ukikaa nao wanakutia unyonge, wana lalamika kila wakati - hii inasababishwa na kushushwa kwao thamani, eitha kwa fikra zao wenyewe au mtu au watu walio wazunguka. Kila mara watu hawa hujilinganisha na wengine (tena utakuta baadhi yao ni wacha Mungu sana), kufanya hivyo ni njia kubwa ya kushusha thamani yako. Unapo waangalia wengine na kufikiri kuwa “kwa nini mimi nisiwe kama fulani, mbona Mungu anampendelea hivyo”, pindi tu unapoanza kuwa na fikra kama hizi, basi jua kuwa umeshaukoleza moto wa kuushusha utu wako na utajisikia vibaya tu! Na pia kuna watu ambao ni eitha wenye kipato cha chini kabisa au walemavu, lakini ukikaa nao katika mazungumzo unakuwa na furaha sana kwa kuwa ni wachapa kazi, wacheshi, wanajiamini, wanauthamini utu wao, hawalalamiki na wanayakubali maisha waliyonayo na kukabiliana na kila hali, tena maisha yao yamejaa amani kuliko unavyotarajia. Yote ni juu ya kutumia mbinu hizi za kujithamini na kujiamini.

Tembelea ukurasa wetu wiki ijayo kuanzai Jumatatu tukijaaliwa tutakuletea mlolongo mzima wa mbinu ambazo zitakusaidia jinsi ya kujijengea tabia za kujiamini na kuachana na mawazo HASI ya kujishusha thamani. Tunakutakia siku njema!
Read More ...

0 comments

MTU yeyote aliyevunjika moyo au kukata tamaa kutokana na mambo magumu yaliyompata, iwe ni kuyumba kiuchumi, kufiwa na ampendaye, kukimbiw
a na watoto, maradhi yasiyotibika au kuachwa na mume au mke, huwa anapata maumivu makali yanayokata kama kisu ndani na hata kuathiri hisia, fikra pamoja na maamuzi anayoweza kuyafanya. Maisha yaliyojaa utoshelevu na mafanikio na uwezo wa kupata kila kitu cha muhimu unachokihitaji, ikiwa ni pamoja na ndoto zako nyingi kutimizwa, yaweza kubadilika kabisa na kuwa kinyume cha hapo kiasi cha kufanya mtu ahisi hana sababu tena ya kuishi iwapo sababu au vigezo vyote vilivyokuwa vikikupa utoshelevu na furaha vimetoweka! Watu uliowazoea na kushirikiana nao wanaweza kukutenga au kukushusha hadhi mara wagunduapo kuwa meli yako yakaribia kuzama, iwe ni kiuchumi, kijamii au kiafya. Inaaminika kuwa haijalishi ni sababu gani kubwa iliyomfanya mtu kukata tamaa ya maisha, kuvunjika moyo, au kuwa na msongo wa mawazo. Njia inayotumika ili kuponya na kurejesha katika uzima na ubora wa maisha ni ile ile kwa kila mtu. Mungu hafurahishwi na kushindwa kwetu, naye huumia pamoja nao wanaoumia lakini yupo tayari kuponya vidonda vyote vilivyoshindikana kupona ili kufanya upya tena. Madaktari husema mfupa uliovunjika ukiunga unakuwa na nguvu zaidi pale palipokuwa pamevunjika kuliko sehemu nyingine za huo mfupa. Ndivyo ilivyo hata kwa mtu aliyekata tamaa na kuvunjika moyo anapokubali kuchukua hatua za kupambana na hali yake hiyo, mwisho wa siku aweza kuwa mwenye nguvu na bora kuliko alivyokuwa hapo awali. Hebu tuangalie kanuni za kukabiliana na hali ya kukata tamaa. Kwanza yatakiwa ukubaliane na zile hali ambazo huwezi kuzibadili tena. Kumbuka yapo mambo katika maisha yako, hata ungejaribu kwa jitihada kubwa sana kuyabadili usingaliweza. Mfano: Huwezi kubadili hali ya hewa, huwezi kubadili majira au mzunguko wa saa, huwezi kubadili yaliyokwisha kupita, Huwezi kubadili ukweli kwamba umpendaye kakutoka na mambo mengine yafananayo na hayo. Wakati mwingine waweza kulazimika kukubaliana na majibu ya kukatisha tamaa ya daktari yanayoashiria mwisho wa maisha au ugonjwa usio na tiba lakini bado ukiwa na amani moyoni na kumuachia Mungu aamue, waweza kukubaliana na matokeo. Ufunguo wa amani moyoni ni pale unapokubali kuwa huwezi kubadili matatizo mengine bali waweza kuacha mikononi mwa Muumba ambaye ni mkuu kupita wote. Muombe Mungu akujalie neema kukubaliana na vile usivyoweza kuvibadili pia akujalie nguvu kubadili vile unavyoweza na hekima ya kujua utofauti. Yakupasa kusimama ili kukabiliana na changamoto yako mwenyewe. Kamwe usikimbie matatizo! Hakuna mtu yeyote anayependa kuaibika, kuaibishwa au udhaifu wake kuanikwa hadharani kwa kila mtu kuuona, zaidi sana inapokuwa kwamba yeye ni mtu mwenye heshima au dhamana katika jamii yake aliyopo. Mfano: Wakati mwingine tunajitwika lawama tusizostahili ili tu kuhalalisha au kubadili mwonekano halisi uwe tofauti. Tupo tayari kuingia gharama iwayo yoyote kuzuia au hata kuahirisha matukio ya uchungu maishani, lakini mara nyingi hizi huwa ni mbio za sakafuni ambazo huishia ukingoni. Kamwe usikimbie changamoto zinazokukabili kimaisha. Simama kidete kubaliana na ukweli halisi ya kwamba mambo mengine huwezi kuyabadili bali kuyakubali. Mtu huheshimika kwa jinsi awezavyo kukabiliana na changamoto zake mwenyewe za maisha. Fahamu kuwa huwezi kubadili mitazamo ya watu wengine juu yako. Waweza kubadili mtazamo wako mwenyewe na matendo yako, na hapo ndipo watu wanaokuzunguka watakapobadili mitazamo yao juu yako kutokana na badiliko lako. Mfano: Iwapo unataka jamii ikuchukulie kama mtu anaye jiheshimu, mkarimu au mwenye kujithamini ni lazima na wewe mwenyewe uishi kama unavyotaka watu hao wakuchukulie. Huwezi kutegemea kuheshimiwa na watu iwapo wewe mwenyewe haujiheshimu au hauthamini utu wako. Watu wengi hupenda kuheshimiwa au kusifiwa hata kwa mambo ambayo hawastahili au hawajayafanya; kwa kisingizio cha cheo au dhamana katika jamii husika. Lakini mwisho wa siku ukweli unapokuja kudhihirika, unakuwa umeshusha kabisa hadhi na dhamana yake katika jamii. Hivyo uponyaji wa kihisia unaanza pale unapochukua hatua kubwa ya kwanza ya kukubaliana na hali halisi juu ya vile vitu ambavyo huwezi kubadilisha. Kukubali inamaanisha kuacha kuzuia yasiyozuilika. Mfano, huwezi kumlazimisha mtu kufanya asiyotaka kufanya. Huwezi kubadili kifo au ugonjwa nk. Kukubali huondoa maumivu mengi yaliyojificha na kuchukua uchungu na maumivu moyoni. Ikubalike tu kwamba unapoacha kujitaabisha kwa mawazo, hali ya kuchanganyikiwa hutoka na hapo ndipo mwisho wa mateso na mwanzo wa amani. Kuna amani ipitayo ufahamu wa kibinadamu ambayo Mungu hutoa kwa wale wote wanaokubali kumwachia nafasi. Usijisumbue kwa jambo lililo nje ya uwezo wako kwani utashindwa kufurahia maisha kwasababu ya kufikiri sana mambo usiyoweza kuyabadili. Mfano, mambo madogo kama mvua itanyesha au jua litawaka, si juu yako kujitaabisha nayo. Simama imara, kusanya nguvu zako na kabiliana na changamoto zako. Acha kujitesa kwa mawazo na ukubaliane na hali halisi unayoipitia. Hakuna mafanikio pasipo maumivu. Mbali na maumivu unayokutana nayo hutokea mabadiliko ambayo husababishwa na kuachwa na mke, familia au watoto. Watu huweza kubadilika kutokana na jinsi ulivyo, kwa kuwa hautakuwa kama ulivyokuwa siku iliyopita. Na kwa uwezo wa Mungu unaweza kubadilika na kuwa mtu mzuri zaidi kwa siku zijazo. Usijaribu kubadili tabia ya mtu mwingine. Kwa msaada wa Mungu, atakusaidia kuibadili tabia yako. Unaweza ukaibadili tabia yako, unaweza ukabadili ustaarabu wako, unaweza ukabadili tabia mbaya ikawa nzuri, unaweza ukaibadili kazi yako, unaweza ukabadili ndoa yako ingali mapema na waweza ukabadili moyo uliovunjika. Kila siku watu hubadilika, kwa msaada wa Mungu katikati ya watu wazuri hufanywa imara kuliko hali ya kukatishwa tamaa uliyokuwa nayo.
Read More ...

0 comments

Ili kuwa mtu wa mafanikio ni vema kutumia mbinu ya kufikiri kwa ubunifu kile unachotaka kukifanya.
Ni vizuri kuwa na imani, unaweza kufanya jambo lako na likafanikiwa, kwani unapoamini litafanikiwa, akili yako itazidi kutafuta njia ya kulifanikisha zaidi.
Kuamini kuwa unaweza kufanya jambo kubwa, kunafungua njia ya mafanikio. Kamwe usiseme ama kufikiri kuwa huwezi kufanya jambo fulani katika maisha yako, badala yake, jaribu kufanya kile unachofikiri kuwa huwezi.
Usiruhusu mambo ya mila na desturi ama utamaduni uliouzoea kutawala akili yako.
Kuwa mtu wa kupokea mambo na mawazo mapya kila wakati, kisha uyafanyie kazi.
Kila wakati jaribu njia mpya katika kufanikisha mambo yako, pamoja na kuwa mfuatiliaji wa shughuli zako unazozifanya.
Iulize nafsi yako, inakupasa kufanya nini ili kuweza kufanya vizuri zaidi? Wakati unajiuliza swali hilo, unakuwa tayari umeshapata jibu, cha msingi ni kulifanyia kazi jibu hilo ulilolipata bila kuchelewa.
Pia jiulize ni kwa vipi unaweza kufanya vizuri zaidi? Pia ni vema ukawa na mazoea ya kusikiliza na kuuliza kwa wengine, kuhusu mambo unayotaka kuyafanya kwani utapata mawazo mengi usiyoyajua kutoka kwa wengine.
Yapanue mawazo yako, kwa kujichanganya na watu mbalimbali wakiwamo wenye ujuzi wanaoweza kukupa mawazo na njia mpya za kufanya mambo.
Moja ya kanuni ya mtu anayependa au mwenye mafanikio ni kuwa na muonekano mzuri mbele ya jamii, kuanzia anavyozungumza hadi mavazi yake.
Unaweza usikubaliane nami, lakini ukweli ni kuwa, kama wewe ni mfanyabiashara wa nguo, jinsi unavyokuwa mtanashati mbele za watu, ndivyo watakavyopenda kuja katika duka lako na kununua bidhaa zako hizo.
Lakini, kama utakuwa haujijali kwa upande wa mavazi, halafu ukawa mfanyabiashara wa bidhaa hiyo, utapata wateja wale wasiokujua na wanaokujua wachache.
Utanashati unavutia biashara yako, si tu kwa biashara ya nguo, bali hata katika shughuli zako nyingine unazozifanya, uwe ni mwanasheria, mwalimu ama mpishi wa chakula, vile unavyoonekana ndivyo unavyozidi kuimarisha biashara yako.
Kumbuka watu wanakutathmini kutokana na muonekana ulio nao.
Hebu tuangalie mfano huu kuwa, mtu anafanya biashara ya nyanya, anazipanga mafungu mafungu na kuziuza.
Mwingine anafanya biashara hiyo hiyo, na kuziweka nyanya zile katika mfuko wenye kuonyesha bidhaa iliyopo ndani yake na kufunga vizuri.
Biashara hizo zikiwa katika eneo moja, watu wengi watanunua zile zilizofungwa vizuri kwenye mfuko wakiamini kuwa ni salama zaidi.
Mfano huo ni sawa na muonekana ama utanashati wako kwa watu katika shughuli yoyote ile unayoifanya.
Uvaaji mzuri na wa heshima kwenye jamii, unakufanya uheshimike na kuaminika kuwa unaweza kufanya mambo makubwa unayoyapanga.
Ni vizuri kuboresha mawazo yako kila siku, kama watu maarufu wanavyokuwa.
Kuboresha mawazo, kufikiri na utendaji wako kutakuletea mafanikio katika mipango yako yote.
Hivyo ni vema, kula vizuri ili uweze kufikiri vizuri katika mambo unayoyafanya.
Endapo hautakula mlo kamili, akili yako haitakuwa na uwezo wa kufikiri vizuri, utabakia kuwa mtu wa kushindwa.
Kama mtu anakula vizuri, anajilinda na magonjwa mbalimbali, mwili wake unakuwa na afya pamoja na akili yake kuwaza mambo makubwa.
Akili yako huwezi kuilisha chakula unachokula, bali chakula chake ni mazingira yanayokuzunguka.
Mtu yeyote anayetembea katika nchi ama mikoa mbalimbali, huwa na mazingira ya tofauti, kila anapokwenda hujifunza kitu kitakachomsaidia.
Mazingira ya eneo ulilopo yanaifanya akili yako ifikiri zaidi ufanye kitu gani cha mafanikio katika eneo hilo ulilopo kitachokupatia maendeleo.
Ukubwa wa jinsi unavyowaza, malengo yako, mazingira yako au vile unavyoonekana, ni kutokana na mazingira uliyopo.
Unapokuwa na watu wenye mawazo ya kuchelewa kufanikisha mambo, nawe utakuwa mtu wa kuchelewa kufikia malengo uliyojiwekea.
Kwa maana nyingine, kushirikiana na watu wenye mawazo makubwa kunakufanya uwaze mambo makubwa ya maendeleo.
Pia kukaa karibu na watu wenye malengo ama maono ya mafanikio, kunakufanya nawe uwe katika hali hiyo.
Katika jamii tunayoishi, kumekuwa na watu wenye tabia zilizogawanyika katika makundi matatu.
Kundi la kwanza, ni la watu wale ambao wameona kuwa hawawezi kufanya jambo likafanikiwa kabisa.
Wamekuwa na ujuzi na kukubali ujuzi huo katika eneo moja, yaani wameridhika na hali hiyo.
Kama, Mungu amekupa ujuzi wako mzuri na ukabahatika kupata kazi sehemu nzuri, pamoja na kufanya kazi ile, utumie ujuzi wako katika maeneo mengine.
Unaweza kufungua ofisi yako na kuanzisha kitu chako mwenyewe huku ukiendelea na kazi yako.
Kamwe usijikatishe tamaa kwa kuona kuwa huwezi kufanya hivyo, kudhani kuwa, wewe umeumbwa kwa ajili ya kufanya kazi za wengine tu.
Kuna watu wenye malengo makubwa na waliopanga kuyatimiza lakini kutokana na ushindani uliopo hufika mahali na kushindwa kuendelea na mikakati waliyojiwekea.
Tunaweza kusema, wamekata tamaa na kuacha kuyafanyia kazi malengo yao, mwishoni hupoteza mwelekeo kabisa.
Kundi hili, wamejijengea tabia ya hofu, hofu ya kushindwa kutimiza malengo yao, hofu ya ulinzi, hofu katika jamii inayomzunguka na kupoteza kila wanalicho nacho.
Kundi la watu hawa, kamwe hawatafanikiwa kwani wameshajiweka kwenye kundi la kushindwa ingawa lina watu wenye akili, vipaji walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Kundi la tatu ni la watu wale ambao hawako tayari kukatishwa tamaa, hawa ni asilimia ndogo sana katika jamii.
Kundi hili pamoja na kukatishwa tamaa, katika mipango yao, wamekuwa wakijitahidi kufanya jitihada mbalimbali ili wajikwamue katika hali hiyo waliyonayo na kuwa katika hatua nyingine.
Mara zote hupumua mafanikio katika maisha yao. Kundi hili pia lina furaha kwa kuwa limeshakamilisha baadhi ya malengo waliyojiwekea.
Wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali, lakini wamezishinda, wamekuwa wakiangalia siku mpya ikianza na jambo jipya.
Ni ukweli usiopingika kuwa, kila mmoja wetu anapenda kuwa katika kundi la tatu, ambalo kila mwaka wanapata mafanikio, wanaofanya mambo mbalimbali na matokeo yake yanaonekana..
Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa kitabu cha 'The Magic of Thinking Big,’ kilichotungwa na David Schwartz pamoja na mitandao mbalimbali.
Read More ...

0 comments


 


Ndugu wadau napenda kumshukuru Mungu kwa mema mengi anayonijalia mimi na wewe kils siku iitwapo leo
ndugu mdau wangu kusoma vitabu ni jambo muhimu sana kwani mambo mengi katika ulimwengu huu yapo katika maandishi zaidi,yaani kwa kifupi goood information zote za dunia hii zipo kwenye maandishi,kwahyo ni jambo la muhimu sana kuanza kusoma vitabu kwani ni mojawapo ya njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha yetu hapa duniani
Ndio maana hata maneno ya mungu yaapo katika vitabu.
ndugu yangu usitegemee kupata habari nzuri kama hauna desturi ya kusoma vitabu najua watu wengi tupo katika pilika mbali mbali za kutengeneza pesa lakini tunapaswa vilevile tutenge na muda wa kujisomea kuongeza mbinu mbalimbali za kutuwezesha kuwa na vipato vizuri,
ndugu yangu mimi huwa naamini mafanikio ya kweli yanapatikana kwenye kusoma vitabu,ndugu yangu naomba kuanzia leo ujenge utaratibu wa kusoma vitabu.
ndugu mdau kama unahitaji kusoma vitabu vizuri vya kukujengea misingi imara ya maisha yako unaweza kuniandikia email alafu nikakushauri ni vitabu gani vizuri vya kusoma na vilevile naweza pia kukutumia kitabu kwenye email yako na wewe ukafaidi hiki ninachokiandika hapa
Read More ...

0 comments